Nafasi Ya Matangazo

September 02, 2013


Redd’s Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa (19) akipozi kwa p[icxha mara baada ya kuibuka mshindi wa taji hilo na kuwa mrembo wa kwanza kutinga nusu fainali za Miss Tanzania 2013 baada ya kuwashinda warembo wenzake 29 katika shindano hilo dogo kuelekea fainali za Redd’s Miss Tanzania 2013. 
********   ********
Mrembo wa Mkoa wa Dodoma,  na mwakilishi wa Kanda ya Kati, Happiness Watimanywa, juzi amenyakua taji la Redds Miss Tanzania Photogenic 2013 na kuwa  mrembo wa kwanza kuingia hatua ya nusu fainali ya shindano la Redds Miss Tanzania 2013. 


Happiness amefanikiwa kuingia hatua hiyo ambayo itaingiza warembo 15 bora na kuwashinda warembo wenzake 29 ambao wapo katika kambi ya Redds Miss Tanzania 2013.

Shindano hilo dogo la Haiba ya Picha “Miss Photogenic” alipatikana baada ya jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha mashuhuri nchini Tanzania wakiongozwa na Jaji Mkuu Mroki Mroki kutoka magazeti ya Serkali Daily News, Habarileo na Spotileo.

Mapema akitaja majina ya warembo walioingia hatua ya tano bora Mroki aliwataja mamaji wengine aliyoshirikiana nao kuwa ni Mpigapicha wa Jambo Leo Richard Mwaikenda na Mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Aika Kimaro.

Dalili za kuonesha kuwa Happiness amekubalika hata kwa washiriki wenzake katika shindano hilo ziliibuka wakati Mroki akitaja majina ya warembo waliofanikiwa kuingia hatua hiyo na lilipotajwa jina lake katika Hoteli ya Giraffe Ocean View warembo ulilipuka kwa kwashangwe.

Warembo watano walifanikiwa kuingia katika mchujo huo ni pamoja na Anastazia Donald ,Latifa Mohamed, Clara Bayo na Jacline Luvanda na Happiness Watimanywa aliyeibuka mshindi.

Warembo wa Redds Miss Tanzania watashindana tena katika shindano la Miss Top Model linalotaraji kufanyika Septemba 7 mwaka huu, katika Hotel ya Naura Spring jijini Arusha.

Mataji mengine yatakayo waniwa na warembo hao na washindi kuingia moja kwa moja klatika hatua ya Nusu fainali ni Miss Talent, Miss Personality na Miss Sports Woman.

Taji la Miss Photogenic lilikuwa linashikiliwa na mrembo Lucy Stephano kutoka Manyara na Kanda ya Kaskazini, kutoka Shinyanga na Kanda ya Ziwa. 

Fainali za mwaka huu za Redds Miss Tanzania zinataraji kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City  jijini Dar es Salaam Septemba 21,2013.
Mrembo Happiness Watimanywa akiwa amekubwa na butwaa baada ya kutajwa Mshindi wa Redd's Miss Photogenic 2013. 

Redd’s Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa (katikati) akipozi kwa picha na warembo wengine walioingia hatua ya tano bora ya kumsaka mshindi wa taji la Miss Photogenic 2013. Kutoka kulia ni Anastazia Donald ,Latifa Mohamed, Clara Bayo na Jacline Luvanda.(
Warembo wengine Walioshiriki shindano hilo wakifuatilia utangazwaji wa matokeo hayo katika Hoteli ya Giraffe Ocean View katika kambi yao. 
Posted by MROKI On Monday, September 02, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo