Nafasi Ya Matangazo

March 03, 2015

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Teknolojia mpya ya umeme jua ya gharama nafuu ijulikanayo kama 3G+Solar Homes System (SHS). Katikati ni Paul Kiwele Naibu  Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini,Mwisho ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam.
Mgeni rasmi katika uzinduzi  wa Teknolojia mpya ya umeme jua ya gharama nafuu ijulikanayo kama 3G+Solar Homes System (SHS) Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini Paul Kiwele katikati akizindua teknolojia hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam
 Injinia Arnold Swai wa Kampuni ya Rex Energy akionyesha namna  Teknolojia mpya ya umeme jua ya gharama nafuu ijulikanayo kama 3G+Solar Homes System (SHS) inavyofanya kazi. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa na Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini Paul Kiwele.
Mwandishi wa habari kutoka kituo cha televisheni cha channel 10 Peter Shedrack akipokea zawadi ya solar mpya aina ya 3G+Solar Homes System (SHS)  aliyojishindia wakati wa droo iliyochezeshwa kwenye uzinduzi wa teknolojia hiyo jijini Dar es Salaa. Anayemkabidhi ni Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini Paul Kiwele na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa.
Waandishi wa habari waliojishindia seti ya mfumo mpya wa umeme jua ujulikanao kama  3G+Solar Homes System (SHS) kwenye droo iliyochezeshwa wakati wa uzinduzi jijini Dar es Salaam jana. Wa kwanza kulia (waliovaa suti) ni   Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam alikifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa na mgeni rasmi katika uzinduzi huo Paul Kiwele ambaye ni Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini
Posted by MROKI On Tuesday, March 03, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo