Nafasi Ya Matangazo

February 07, 2015

Lucas Mpira maarufu Google enzi za uhai wake.
VILIO, majonzi na simanzi ya hali ya juu vimetawala  kwa wakazi wa wa Kipungini A, Ukonga banana jijini Dar es Salaam kufuatia vifo vya watu sita wa familia moja vilivyotokana na ajali ya moto.

Vifo hivyo ni vya familia ya Kapteni mstaafu wa JWTZ, David Mpira na Mkewe Selina Yegela ambae pia ni mstaafu wa DAHACO siku hizi Swissport waliokufa baada ya nyumba walio kuwa wakiishi kuteketea kwa moto alfajiri ya leo.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki na kuwataja waklio poteza maisha katika tukio hilo mbali ya wastaafu hao kuwa ni pamoja na  Lucas Mpira na Samwel Yegela ambao ni watoto wao.

Pia wapo wajukuu wawili wa Mzee Mpira waliotambulika kwa majina ya Selina Emmanuel (9) ambaye anasoma darasa la pili Shule ya Msingi Minazi Mirefu na Pauline Emmanuel (3), anaesoma chekechea Shule ya Tumaini  ya Kitunda. Maiti wote wamehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Waombolezaji wakilia kwa uchungu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya akiangalia nyumba hiyo.
Posted by MROKI On Saturday, February 07, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo