Nafasi Ya Matangazo

January 29, 2015

Wanachama 30 wa Chama cha Wananchi CUF, leo wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na kusomewa mashitaka matatu yanayo wakibili.

Washitakiwa hao waliofikishwa mbele ya Hakimu Mkazi, Emmilius Mchauru wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu walisomewa mashitako hayo matatu ambayo ni Kula njama ya kufanya jinai kesi inayowakabili watuhumuwa wote 30 kosa walilolitenda huko Temeke. 

Kosa la pili ni kufanya mkusanyiko usio halali na kosa la tatu ni kufanya mgomo wa katazo halali la Jeshi la Polisi ambapo kosa la pili na tatu linawakabili mtuhumiwa wa kwanza hadi 28.

Masharti ya dhamana yalikuwa wazi kwa watuhumiwa hao. 

 Ulinzi mkali wa polisi kwa watuhumiwa hao ambao walipelekwa rumande wakati mchakato wa dhamano yao ukifanyika ambao kila mmoja anatakiwa kusaini dhamana ya shilingi 100,000/= pamoja na mdhamini mmoja.
Ndugu na jamaa wakipata maelekezo kutoka kwa watuhumiwa hao.
Posted by MROKI On Thursday, January 29, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo