Nafasi Ya Matangazo

December 11, 2014

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Maimuna Tarishi (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Grace Daffa, wakionesha vitabu vyenye ripoti ya mwaka mmoja ya watoto waliopo magarezani jijini Dar es Salaam kutokana na kukinzana na sheria, baada ya kuzindua ripoti hiyo Dar es Salaam leo.  Ripoti hiyo imefanyiwa utafiti na kituo hicho kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef).
  Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Grace Daffa (kulia), akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo. Kushpoto ni  Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Grace Daffa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Maimuna Tarishi.
 Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
  Maofisa wa WLAC wa kwenye uzinduzi huo.
 Wahisani wa WLAC nao walijumuika kwenye hafla hiyo.
Mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba naa Sheria (katikati walio kaa, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa uzinduzi huo.
******
Dotto Mwaibale
SERIKALI imesema kuna kazi kubwa katika kukabiliana na changamoto za utoaji wa msaada wa kisheria kwa watoto wanaokinzana na sheria hapa nchini.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mwaka mmoja ya watoto wanaokinzana na sheria, Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Maimuna Tarishi alisema hiyo ni moja kati ya changamoto zinazowakabili wakati wa utoaji wa msaada wa kisheria kwa watoto hao.

Alitaja changamoto nyinmgine ni kukosekana kwa miundombinu ya kushughulikia mashauri ya watoto hao kwa kutokuwepo kwa mahakama maalumu za kutosha kwa ajili ya kusikiliza mashauri ya watoto , mahabusi za watoto.

Nyingine ni maafisa wa ustawi wa kutosha katika mahakama zote za wilaya na mwanzo, ambapo pia watoto wanaweza kushitakiwakutokana na sababu mbalimbali za kisheria, ufunguaji wa kesi za watoto kwenye mahakama nyingine badala ya watoto na uwepo wa watoto wengi wasio na makazi na hatimaye kujikuta wanarudia kufanya makosa.

Akizungumza wakati akiwakilisha taarifa hiyo Wakili wa Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa wanawake, Juvenal Rwegasilaalsema kwa kipindi cha mwaka huo kituo hicho kimefanikiwa kuwahudumia kesi 115 za watoto kutoka kwenye mahakama mbalimbali ambao wametoka katika mahabusi za Segerea, keko na upanga.

Alisema licha ya mafanikio hayobado wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ambazo ni ugumu wa kupatikanaji wab taarifa sahihi kwa kesi za watoto, kesi kuchukua muda mrefu na baadhi ya watioto kudanganya umri.

Mbali na hilo pia lisema katika sehemu kubwa ya jamii na wazazi wa watoto wengi wao wamekuwa hawajui haki za watoto hivyo kusababisha kesi kufutwa kwa kupewa fungu la fedha.

Alisema kwa sasa ni vyema elimu itolewe kuhusu haki za watoto, malezi sahihi kwa watoto. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari zajamicom)
Posted by MROKI On Thursday, December 11, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo