Nafasi Ya Matangazo

October 01, 2014

Jambazi mmoja auawa na wananchi baada ya kumpora mwananchi mmoja kiasi cha Sh.2,100,000= wa kijiji cha Igoji One Kata ya Mima katika Wilaya ya Mpwapwa.

         Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma ameeleza kuwa tukio hilo la kumvamia mwananchi huyo huko nyumbani kwake Igoji one aliyejulikana kwa jina la YARED S/O MAPATANO MSALILA lilitokea mnamo tarehe 28.09.2014 majira ya saa 22:00 usiku na kisha kupora kiasi hicho cha fedha na kumjeruhi sehemu za kichwani na mguuni.

         Baada ya kufanya tukio hilo wakiwa wanne, wananchi waliwafuatilia toka Igoji one Mpwapwa wakishirikiana na wanakijiji wa Iwendo na Fufu na kufanikiwa kumkamata jambazi mmoja baada ya kumjeruhi mwananchi mmoja VICENT S/O MAKALI kwenye kidole cha shahada cha mkono wa kushoto kwa risasi wakati wanamnyang’anya jambazi huyo bastola aliyokuwa nayo. Wananchi hao walifanikiwa kumnyang’anya bastola hiyo yenye namba DAA 317086 aina ya Bereta ambayo imegundulika kuibiwa huko Tuangoma Kongowe Temeke Dar es Salaam tarehe 19.04.2014 walipomvamia SHADRACK MUGALULA nyumbani kwake na kumpora silaha hiyo. 

Baada ya wananchi kuona kuwa mwananchi mwenzao amejeruhiwa ilibidi wajihami na kumshambulia jambazi huyo kitendo kilichomfanya kupoteza maisha. Jambazi huyo ametambuliwa kwa jina la LAMECK S/O CHARLES @ LUMOLWA, MGOGO, MIAKA 30, MKAZI WA KIJIJI CHA MBABALA Wilaya ya Dodoma.

Kamanda wa Polisi amesema kuwa majambazi wengine watatu wanaendelea kusakwa ili waweze kufikishwa mahakamani.
Posted by MROKI On Wednesday, October 01, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo