Nafasi Ya Matangazo

October 01, 2014



Rama Salim (kushoto) akiwania mpira na Emmanuel Okwi wa Simba.
Na Fadher Kidevu Blog
KIUNGO wa Coastal Union  Mkenya Rama Salim amesema yeye ni zaidi ya Haruna Niyonzima na Pierre Kwizera wanaochezea klabu kongwe za Simba na Yanga

Rama Salim amesema licha ya nyota hao kutoka nchi za Burundi na Rwanda kuwa na majina makubwa lakini wanamchango mdogo kwa timu hizo tofauti na uwezo wao wanapokuwa uwanjani

“Pengine majina yao yanatokana na ukubwa wa timu wanazochezea lakini uwanjani hawana tofauti nanigumu kushindana na mimi kwa sababu nimewaacha mbali na kazi yangu inaonekana ndani ya timu.

Rama Salim amejiunga na Coastal msimu huu akitokea Gor Mahia ya Kenya na tayari ameifungia timu hiyo bao moja katika mechi dhidi ya Simba ambapo tiu hizo zilitoka sare ya 2-2 kwenye mechi ya ufunguzi ya msimu huu uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Wednesday, October 01, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo