Nafasi Ya Matangazo

September 30, 2014



Na Fadher Kidevu Blog
KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mart Nooij ameita kikos cha wachezaji 26  kwa ajili  ya mechi ya kirafiki iliyopo kwenye Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa ya FIFA dhidi ya Benin ambayo itachezwa  Oktoba 12 uwanja wa taifa Dar es Salaam.

Kocha Mart Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Mpirawa Miguu Afrika (CAF), amesema mchezo huo ni muhimu kwa Tanzania kushinda ili kurudisha matumaini kwa mashabiki wake ambao wamekata tamaa baada ya kutolewa katika mshindano mbalimbali ikiwemo yale ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika ambazo zitafanyika Morocco mwakani.

“Benin ni timu nzuri ambayo itatupa mazoezi mazuri lakini kurudisha imani kwa mashabi wetu ambao wamepoteza matumaini na sisi,”amesmea Nooij.

Kikosi hicho kinatarajia kuingia kambini Oktoba 6 na wachezaji walioitwa kwenye kambi hiyo kwa upande wa makipa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam).

Mabeki ni Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).

Viungo ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna Chanongo (Simba).

Washambuliaji ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).
Posted by MROKI On Tuesday, September 30, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo