Nafasi Ya Matangazo

April 16, 2014

Mshambuliaji wa Shule ya Sekondari ya BaoBab ya Bagamoyo mkoani Pwani, Zuward Ally akiwatoka mabeki wa timu ya Upendo wakati wa Tamasha la Soka la kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani 2014 lililoandaliwa na IDYDC na Grassrootsoccer kwa udhamini wa ExxonMobil, katika Uwanja wa Kituo cha Soka la Matumaini cha FIFA, mjini Iringa Mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo lilihusisha wachezaji 80 vijana wa kike wenye umri kati ya miaka 15 - 18 kutoka timu nane za Bagamoyo na Iringa. Upendo ilishinda bao 1-0. PICHA ZOTE NA JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG
Mchezaji wa timu ya Upendo, Felista Ngimbuchi (kulia), akiwatoka wachezaji wa Shule ya Sekondari ya BaoBab ya Bagamoyo mkoani Pwani, wakati wa Tamasha la Soka la kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani 2014, lililoandaliwa na IDYDC na Grassrootsoccer kwa udhamini wa ExxonMobil katika Uwanja wa Kituo cha Soka la Matumaini cha FIFA, mjini Iringa jana. Tamasha hilo lilihusisha wachezaji 80 vijana wa kike wenye umri kati ya miaka 15 - 18 kutoka timu nane. Upendo ilishinda bao 1-0.
Beki wa timu ya Mshindo, Anifa Kalinga (kulia), akimtoka mshambuliaji wa timu ya Nianjema, Zainab Maulid wakati wa Tamasha la Soka la kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani 2014, lililoandaliwa na IDYDC na Grassrootsoccer kwa udhamini wa ExxonMobil katika Uwanja wa Kituo cha Soka la Matumaini cha FIFA, mjini Iringa jana. Tamasha hilo lilihusisha wachezaji 80 vijana wa kike wenye umri kati ya miaka 15 - 18 kutoka timu nane. Mshindo ilishinda kwa bao 2-1.


Posted by MROKI On Wednesday, April 16, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo